Jumapili 23 Novemba 2025 - 23:28
Waandamanaji Wanaotaka Amani Watawanywa na Polisi Uingereza

Hawza/ Polisi wa Uingereza kwa mara nyingine imewatawanya kwa nguvu waandamanaji wapenzi wa amani na kuwakamata baadhi yao. Waandamanaji hawa walikuwa wakipinga hukumu ya mahakama iliyopiga marufuku shughuli za kundi la wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina, na walikuwa wamefanya maandamano ya kimya kimya mbele ya jengo la mahakama mjini London kwa kuonesha vipeperushi na maandiko.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, waandamanaji walikuwa na mabango yaliyoandikwa: "Mimi napinga mauaji ya kimbari. Mimi ninaunga mkono hatua za Palestina." Maandamano yenye kaulimbiu na malengo kama haya pia yalifanyika Jumanne katika miji ya Nottingham, Gloucester, Truro, Northampton, Oxford, Leeds, Newcastle, Cardiff, Aberystwyth na Edinburgh.

Kundi la wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina katika akaunti yao ya X waliandika kuwa: Huda Amori, mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo, anachukua hatua za kisheria dhidi ya uamuzi huo wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza wa wakati huo, na kwamba mbinu ya kulitaja kundi hilo kuwa la kigaidi ni ujanja tu wa kuwatuliza wananchi kwa kuwahadaa.

Chanzo: Shirika la Habari la Anadolu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha